Wataalamu: Vitamini nyingi haziwafai wajawazito

Utathmini mpya wa wataalamu umedokeza kwamba tembe za vitamin mseto zinazopewa wajawazito huwa ni kupoteza pesa bure.Matokeo ya utathmini huo yamechapishwa katika jarida la Drug and Therapeutics Bulletin, ambalo huwafahamisha madaktari na wauzaji dawa Uingereza kuhusu tiba na udhibiti wa maradhi.
Utafiti huo umegundua kwamba vitamini mseto huwa haziwawezeshi kina mama wajawazito na watoto wao kuwa na afya bora na kwamba ni “gharama isiyo na maana”.
Badala yake, wataalamu hao wanapendekeza kwamba wanawake wanafaa kuangazia zaidi kumeza au kunywa vitamin zilizo kivyake ambazo kwa mfano nchini Uingereza hupatikana kwa peni kadha.
Wanafaa pia kula lishe bora na yenye afya.
No comments:
Post a Comment