Saturday, July 16, 2016

WENGER NA PRESHA YA KUWAKOSA MASTAA WAKE UFUNGUZI WA LIGI

Mastaa wa Arsenal watakaokosa Pre Season na mechi ya Liverpool August 14

July 16 2016 kocha wa klabu ya Arsenal ya England Arsene Wenger ametangaza mipango yake kuelekea maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England, Wenger ametangaza mipango yake pamoja na kuwapa mapumziko ya wiki zaidi ya tatu mastaa wake walioshiriki michuano ya Euro 2016.
Mastaa wa Arsenal watakaokosekana katika mechi za maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu pamoja na mechi ya ufunguzi wa Ligi dhidi ya Liverpool August 14 2016 ni  Olivier Giroud, Laurent Koscielny, Mesut Ozil na Aaron Ramsey. Wenger ametoa mapumziko kwa mastaa wake wote waliocheza Euro hadi hatua ya nusu fainali.
150923
Kwa upande wa Jack Wilshere ambaye timu yake ya England ilitolewa katika hatua ya 16 ya michuano ya Euro 2016, amerudi kuungana na Edion Zelalem, Joel Campbell, Gabriel, Stephy Mavididi, Jeff Reine-Adelaide, Mohamed Elneny, Calum Chambers, Chris Willock, Krystian Bielik, Francis Coquelin na Emiliano Martinez.
150928
“Wachezaji walioshiriki michuano ya Euro hadi katika hatua ya ya fainali wanahitaji mapumziko marefu ili waweze kurudi katika hali yao ya kawaida, yanaweza yakawa mapumziko ya zaidi ya wiki tatu, wanabidi wapate muda wa kutosha ili kurudi katika hali ya kawaida na kusahau machungu ya kukosa Kombe la Euro” >>> Wenger
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment