Tuesday, November 1, 2016

SUMYA NYOKA NI DAWA YA KUMALIZA UCHUNGU KWA BINADAMU

Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu

Sumu yake itatumika kutengeneza dawa ya kumaliza uchungu
Joka mwenye sumu kali zaidi duniani huenda akawa jibu la kupatikana dawa ya kupunguza uchungu. Hii ni kwa mujibu ya wanasayansi.
Joka anayejulikana kama 'Blue Coral' ndiye mwenye sumu kali zaidi na hupatikana zaizi Kusini Mashariki mwa Bara Asia. Utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la afya la Toxin umepata joka huyo huwalenga maadui wake ambao husababisha uchungu kwa binadamu.
Wanasayansi wanasema huenda sumu hii ikatumika kutengeneza dawa ya uchungu. Baadhi ya wanyama ambao sumu yao imetumika kutengeneza dawa ni pamoja na konokono wa baharini na bui bui wa sumu.
Wanasayansi sasa wanataka joka huyu kuhifadhiwa hususan baada ya maeneo mengi anakopatikana kugeuzwa kuwa mashamba ya michikichi. Wanasayansi walifanya utafiti wao katika nchi za China, Singapore na Marekani.
Watafiti wanasema japo kwa mwanadamu nyoka huwa adui, lakini wakati huu huenda akawa suluhu la matatizo mengi ya kiafya.

No comments:

Post a Comment