Monday, February 20, 2017

ARSENAL YAIBUKA NA KUSHINDA FA CUP

Sutton United vs Arsenal FA Cup, Theo Walcott kafunga goli la 100

Usiku wa February 20 2017 timu ya Arsenal ilikuwa katika uwanja wa ugenini kucheza mchezo wake wa round ya tano ya FA Cup dhidi ya Sutton United inayoshiriki Ligi daraja la tano England, Sutton United imeingia uwanjani ikiwa nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi daraja la tano.

Arsenal wanaingia katika mchezo huo kocha wao Arsene Wenger akiwa kaandamwa na maneno, toka afungwe goli 5-1 dhidi ya FC Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa Alianz Arena, ushindi wa Arsenal dhidi ya Sutton unaifanya Arsenal kukutana na Lincoln City robo fainali ya FA Cup.

Mchezo dhidi ya Sutton United haukuwa mwepesi sana kwa Arsenal, kwani licha ya kuutawala mchezo kwa asilimia 67 na Sutton wakitawala kwa asilimia 33, haikuisaidia Arsenal kupata ushindi wa idadi kubwa ya magoli na wameishia kupata ushindi 2-0 zilizofungwa na Lucas Perez dakika ya 27 na Theo Walcott dakika ya 55 ambapo hilo linakuwa goli lake la 100 toka ajiunge na Arsenal 2006.

No comments:

Post a Comment