Friday, February 17, 2017

MAKAME ACHEKELEA KUZIDUNDA TIMU ZA TANGA MJINI



Tangakumekuchablog
Tanga, TIMU ya Korogwe United ya Korogwe  mjini imendelea kugawa dozi kwa timu za Tanga mjini kwenye kinyang’anyiro cha ligi ya Mkoa baada ya kuifunga timu ya Sports Prison goli moja.
Kocha wa timu hiyo yenye maskani yake Korogwe mjini, Salim Juma Makame amesema siri ya ushindi mfululizo kwa timu za Tanga ni wachezaji wake kuwaweka katika kambi na kutowaruhusu kutoka nje ya kambi bila dharura maalumu.
Alisema huwa anapata muda mwingi wa kuwafundisha mbinu za ushindi wakiwa kambini na kuwafanyisha mazoezi kutwa mara tatu  bila mchezaji kukosa.
“Furaha yangu ya kuzifunga timu za Tanga mjini haina kifani  na siri kubwa ni kuwaweka pamoja wachezaji wangu na huwa siwaruhusu kutoka nje bila dharura maalumu” alisema Makame na kuongeza
“Ila sio jambo rahisi kuzifunga kwani nao wanacheza mpira mkali wa kuvutia ila nimebaini kuwa kuwaweka pamoja unatengeneza saikolojia fulani ya uchezaji” alisema
Aliwataka wachezaji wake hao kuendeleza ushindi mfululizo kwa kuamini kwamba timu ambayo inakutana nayo ni kuibuka na ushindi mfululizo.
Kwa upande wake kocha wa Sports Prison, Maneno Loya, alisema wachezaji wake hawakuwa makini hasa kwa upande wa beki na kuruhusu goli lililofungwa na mshambuliaji wao Veso Salim kipindi cha pili cha mchezo.
Alisema hana furaha kuona kufungwa mbele ya washabiki wa nyumbani hivyo kuwataka kuwapa moyo kwa kuamini kuwa mchezo ufuatao watajipanga na kushinda.
‘Niseme ukweli sina furaha kufungwa katika uwanja wa nyumbani mbele ya washabiki wanaokushangilia , ila niseme kuna kosa tulilifanya na kuruhusu bao” alisema Loya
Aliwataka washabiki hao kusahau kipigo hicho badala yake kuwaombe dua ili kuweza kushinda na kubeba kombe hilo la ligi ya Mkoa Tanga.
                                 

 Wachezaji wa Korogwe FC wakigombea mpira na mchezaji wa Sports Prison ya mjini Tanga wakati wa ligi ya Mkoa nane bora wakati zilipokutana uwanja wa Mkwakwani juzi ambapo Korogwe FC waliibuka na ushindi wa bao 1.
 Wachezaji wa Korogwe FC wakiondoa hatari langoni kwao wakati wa mchezo wa ligi ya Mkoa nane bora uwanja wa Mkwakwani juzi, Korogwe FC waliibuka na ushindi wa bao 1.
 Wachezaji wa Sports Prison ya Tanga mjini wakimdhibiti mchezaji wa Korogwe FC wakati w amchezo wa ligi ya Mkoa nane bora uwanja wa Mkwakwani juzi, Korogwe FC waliibuka na ushindi wa bao 1.
Mchezaji wa Sports Prison Ali Bayo (88) akitafuta mbinu ya kumtoka mchezaji wa Korogwe FC, Idd Said wakati wa mchezo ligi ya Mkoa nane bora uwanja wa Mkwakwani juzi.

No comments:

Post a Comment