Wednesday, February 8, 2017

FAMILIA YENYE WATU 500 WAFANYA SHEREHE CHINA

Familia yenye watu 500 yapiga picha China

Familia ya Ren yapiga picha kwa pamoja
Zaidi ya jamaa 500 wa familia moja huko China wamepiga picha ya familia.
Picha hizo zilichukuliwa wakati wa kusherehekea mwaka mpya nchini humo ambao huadhimishwa na familia kubwa na vyakula.
Mpiga picha Zhang Liangzong alipiga picha hizo kwa kutumia ndege isiokuwa na rubani karibu na eneo la kitalii la Shishe.
Aliambia BBC kwamba familia ya Ren ambayo inatoka kijijini inadaiwa kuanza miaka 851 iliopita lakini rekodi ya udugu wao haijaangaziwa kwa zaidi ya miongo minane.
Wazee wa kijiji hivi karibuni walianza kuangazia rekodi za familia hiyo na kufanikiwa kupata ndugu wengine 2000 kupitia vizazi saba, alisema  Zhan.
Waliadhimisha mafanikio hayo kwa kuweka mkutano mkubwa na kuweza kupata zaidi ya wanachama 500 wa familia hiyo.
Chifu wa kijiji hicho Ren Tuanjie ameambia chombo cha habari cha Xhinua :Sababu moja ni kuelewa kule wajukuu zao..

No comments:

Post a Comment