Tanga, MKUU wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha
Tumbo amewataka Wajasiriamali wanawake Tanga kulitumia soko la pamoja la Afrika
Mashariki kwa kutafuta masoko na kuacha kutegemea masoko ya ndani.
Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Mkoani
hapa jana, Tumbo alisema soko hilo endapo Wajasiriamali nchini wangelitumia
wangelienuka kiuchumi.
Alisema kazi za mikono ziko na soko kubwa ndani na nje ya
nchi hivyo kuwataka kutambua na kuwa tayari kuyafikia masoko kama ilivyo kwa
wenzao ndani ya jumuiya hiyo.
“Niwambie wajasiriamali wenzangu kwani hata mie pia ni
mjasiriamali ila nadhani niko tofauti na nyie, lilipofunguliwa tu soko la
pamoja sikukumbatia masoko ya ndani” alisema Tumbo na kuongeza
“Nilisafiri na biashara zangu mkononi bila woga na kweli
bidhaa zangu zikawa bora zaidi na kupata wateja wengi ikafikia wao kunifuata
kwangu” alisema
Aliwakumbusha
Wajasiriamali hao kulitumia vyema soko la pamoja kama ilivyo kwa wenzao
jambo ambalo litawawezesha kuwa wajasiriamali wakubwa na wa Kimataifa.
Kwa upande wake Mjasiriamali kikundi cha Twaweza, Aziza Said,
alisema wajasiriamali wengi wa vikundi vyao haviendelei kutokana na kukosa
mikopo ya kujiendeleza.
Alisema kuna baadhi ya taasisi za fedha zinaweka masharti
magumu jambo ambalo limekuwa kukwazo cha vikundi vyao kuendelea hivyo kuitaka
Serikali kusaidia ili kuweza kujikwamua.
“Mikopo imekuwa na masharti magumu sana na kuwa chanzo cha
baadhi ya vikundi kusambaratika na wengine kuhasimiana” alisema Aziza
Ameitaka Serikali Mkoani hapa kuwa mlezi wa vikundi vya
wanawake kuhakikisha wanasonga mbele katika kujikwamua na maisha jambo ambalo
litaepuka na viashawishi vya nje.
No comments:
Post a Comment