Tanga, WAZIRI wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo
na Makaazi, William Lukuvi, amesema mgogoro wa mpaka kati ya Kilindi kwa Tanga na Kiteto kwa Mkoa wa Manyara utapatiwa
ufumbuzi karibuni,
Akizungumza katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin
Shighella na Joel Bendera Mkuu wa Mkoa wa Manyara pamoja na Wakuu wa Wilaya na
Madiwani wa Kilindi na Kiteto, Lukuvi amesema kikao hicho ni agizo la Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa.
Amesema mgogoro huo wa mpaka uko muda mrefu na kusema kuwa awamu hii ya tatu ndio ya mwisho na
hakutakuwa na mpaka mwengine zaidi ya awali wa mwaka 1961 ambao utaboreshwa kwa
kuwekwa alama za kudumu zenye kuonekana kwa mujibu wa makubaliano ya pande zote
mbili.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighella,
amesema kupatikana kwa ufumbuzi wa mpaka huo kutaondosha vitisho na hofu ya
wakulima na wafugaji wa pande mbili hizo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, amesema Serikali
ya Mkoa wake itatoa ushirikiano ili kumaliza mgogoro huo ambao umedumu kwa muda
mrefu.
Mgogoro wa mpaka kati ya Kilindi kwa Mkoa wa Tanga na Kiteto
kwa Mkoa wa Manyara umedumu kwa muda mrefu na kupelekea baadhi ya nyakati kuzuka hali ya Sintofahamu ya wakulima na wafugaji.
Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea Wilaya
mbili hizo Kilindi kwa Mkoa wa Tanga na Kiteto kwa Mkoa wa Manyara na kusikiliza changamoto mbalimbali na mwisho
kuagiza ufumbuzi wa mpaka kati ya Kilindi na Kiteto upatiwe ufumbuzi haraka
No comments:
Post a Comment