HADITHI
ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU
ILIPOISHIA
“Nina hospitali yangu. Ilikuwa ni ya mume wangu, alipofariki
nikabaki nayo mimi”
“Wewe ni daktari?’
“Hapana. Mume wangu ndiye aliyekuwa daktari”
“Hata mimi fani yangu ni ya udaktari”
“Daktari wa nini?”
“Mimi ni daktari bingwa wa upasuaji”
Mwana akamtazama Kweka usoni.
“Sikukutambua. Unafanya kazi aliyokuwa akifanya mume wangu”
“Hivi sasa niko kwenye likizo, ndio sababu nimekuja huku”
“Ninashukuru sana kwa kunifahamisha hilo”
SASA ENDELEA
“Nashukuru umenisaidia, nilikuwa nimechanganyikiwa” Mwana akamwabia
Kweka wakati anaendesha.
“Matukio ya aina ile yanachanganya akili lakini inatakiwa uwe
makini na uchukue hatua za haraka haraka ili kuokoa maisha”
“Ni kweli. Nitampeleka kwenye hospitali yangu”
“Wewe una hospitali?”
“Nina hospitali yangu. Ilikuwa ni ya mume wangu, alipofariki
nikabaki nayo mimi”
“Wewe ni daktari?’
“Hapana. Mume wangu ndiye aliyekuwa daktari”
“Hata mimi fani yangu ni ya udaktari”
“Daktari wa nini?”
“Mimi ni daktari bingwa wa upasuaji”
Mwana akamtazama Kweka usoni.
“Sikukutambua. Unafanya kazi aliyokuwa akifanya mume wangu”
“Hivi sasa niko kwenye likizo, ndio sababu nimekuja huku”
“Ninashukuru sana kwa kunifahamisha hilo”
“Na ni kwanini umeamua kumpeleka kwenye hospitali yako binafsi?”
Alphonce akamuuliza Mwana.
“Kama nitampeleka katika hospitali ya serikali, itabidi niripoti
polisi na sitapenda kesi hii ifike polisi”
“Unataka mmalizane kienyeji?”
“Inatosha”
Baada ya hapo wakawa kimya hadi walipofika katika hospitali hiyo.
Ilikuwa hospitali kubwa kiasi iliyokuwa na majengo ya kupendeza na ya kisasa.
Mwana alisimamisha gari kwenye eneo la maegesho ambalo lilikuwa na magari
kadhaa.
Alifungua mlango akashuka na kwenda kuwaita wauguzi ambao
walifika na machela, wakambeba yule mwanamke na kuingia naye ndani ya majengo
ya hospitali hiyo.
“Twende” Mwana alimwambia Alphonce.
Waliingia katika mlango wa hospitali hiyo wakatokea sehemu ya
mapokezi ambayo waliipita na kutokea katika ukumbi mwembamba wa hospitali hiyo.
“Nisubiri” Mwana alimwambia Alphonce alipofungua mlango wa chumba
cha madaktari na kuingia ndani. Baadaye kidogo alitoka akiwa na madaktari
watatu mmoja akiwa mwanamke.
“Twende” akamwambia Alphonce.
Wakaelekea katika chumba cha matibabu. Wale wauguzi waliokuwa
wamemchukua yule mwanamke walikuwa wakimuingiza kwenye chumba hicho.
“Huyu ni rafiki yangu na pia ni daktari kutoka Tanzania” Mwana
aliwambia wale madaktari.
Madaktari hao wakasalimiana na Alphonce.
Walipofika kwenye mlango wa chumba cha matibabu waliingia wote.
Mwana alikuwa ameshawaeleza madaktari hao kuwa alikuwa amemgonga mwanamke huyo
ambaye alikuwa akiendelea kutapatapa.
Mwanamke huyo alilazwa na kuanza kushughulikiwa. Mwana na Alphonce
walikuwa wamesimama pembeni mwa chumba hicho wakitazama.
Madaktari hao waligundua kuwa damu iliyokuwa ikimtoka mwanamke
huyo ilikuwa ikitoka katika sehemu yake ya kike. Kwa vile ilikuwa ni nyingi
iliwachanganya na kutojua ilikuwa inatokea sehemu gani.
Kwa karibu saa nzima walikuwa wakijaribu kuizuia bila mafanikio.
Wakati wakiendelea na jitihada zao waliagiza awekewe damu nyingine.
“Unaweza kutusaidia?”Mwana alimuuliza Alphonce.
“Naweza”
“Tusaidie”
Kweka aliletewa koti la udaktari akaomba apatiwe mipira ya kuvaa
mikononi.
Alipopatiwa mipira hiyo aliliminyaminya tumbo la mwanamke huyo
kisha akamtazama Mwana.
“Huyo mwanamke anaujauzito ambao umeharibika, anahitajika
kufanyiwa operesheni kuokoa maisha yake”
Wale madakatari waliokuwepo pale wakatazamana. Hawakuwa
wamefikiria jambo hilo.
Alphonce akaagiza vifaa vya kufanyia operesheni. Vifaa hivyo
vilipoletwa alimpasua tumbo yule mwanamke. Alikitoa kichanga cha miezi mine
kilichokuwa kimepoteza uhai kutokana na ajali iliyotokea. Kichanga hicho ndicho
kilichosababisha kuvuja kwa damu.
Alphonce alimsafisha na kumuweka sawa kisha akaanza kumshona.
Alipomaliza alimwambia Mwana.
“Nafikiri tatizo lake limekwisha. Sasa mnaweza kumtibu michubuko”
Dakika chache baadaye mwanamke huyo alikwenda kuwekwa katika
chumba cha peke yake. Alphonce alivua koti la udaktari akampa Mwana.
“Unadhani akizinduka atajisikia vizuri?” Mwana akamuuliza Alphonce
kwa wasiwasi.
“Bila shaka yoyote”
“Tuombe Mungu”
Wakati huo walikuwa wameketi kwenye chumba cha mapumziko. Mwana
akatazama saa yake na kumwambia Alphonce.
“Nimepoteza muda wako mwingi’
“Hakuna tatizo”
“Kwa hiyo nikurudishe hotelini?”
“sawa”
Walitoka na kupanda gari. Walifika hotelini hapo na kukaa kwenye
mkahawa.
“Wakati ule nilikuwa nakuja kunywa supu” Mwana akamwambia
Alphonce.
“Unawza kunywa sasa hivi, nadhani moyo wako umetulia kidogo”
Mwana akaagiza supu na chapati mbili.
“Wewe je?”
“Mimi tayari”
“Ongeza”
“Hapana, ni mpaka saa saba”
Mwana alipoletewa supu na chapatti alianza kunywa.
“Yule mwanamke ningempeleka hospitali ya serikali angekufa” Mwana
alimwambia Alphonce.
“Kama wasingelichunguza kwa makini tatizo lake, angeweza kupoteza
uhai”
“Lakini kwa jinsi ulivyomshughulikia una uhakika kuwa amepona?”
“Yule ameshapona, sina wasiwasi naye”
“Utanipatia namba yako ya simu ili nikupigie kukujulisha hali
yake”
“Nitakupatia, namba yangu ni ya kimtaifa ndiyo ninayotumia hata
nikiwa Tanzania”
“Ni ngapi?”
Alphonce alimpa namba yake. Mwana naye alimpa ya kwake.
Baada ya kumaliza kunywa supu, Mwana aliondoka na kumuacha Kweka.
Saa saba mchana wakati Kweka anakula chakula, Mwana alimpigia
simu.
“Vipi huko?” Alphonce akamuuliza.
ITAENDELEA KESHO hapahapa usikose
No comments:
Post a Comment