Muheza, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha
Tumbo ameitaka jamii kuwasaidia watu wasiojiweza na kuwapa misaada ili kuweza
kuishi katika mazingira mazuri kama wengine.
Akizungumza katika tafrija ya
wazee 58 waliopata tiba ya Upasuaji wa mtoto wa jicho uliofanywa na
madaktari bingwa kutoka taasisi ya Medewell
Health Centre ya Kibaha Mkoani Pwani,
Tumbo amesema wazee wanahitaji uangalizi maalumu.
Ameseme mashirika na taasisi za watu binafsi wanatakiwa kuiga
mfano wa Medewell ili kuhakikisha tatizo la macho kwa wazee na magonjwa mengine
yanatokomezwa.
Akitoa shukrani zake, Mganga Mfawidhi kituo cha Afya cha
Ubwari Health Centre, Rymond Mhina, amesema matibabu yaliyofanyika yalienda
salama kama ilivyokusudiwa mbali ya changamoto ndogondogo kutoka kwa wazee.
Alisema baadhi ya wazee walikuwa woga na kudhani kuwa
matibabu hayo yangewaweka katika mazingira mengine tofauti ambapo wengi
walifurahia na kuona kama zamani.
Akizungumza mara baada ya kufanyiwa matibabu hayo, Lea Stivin
mkazi wa Majengo ameishukuru taasisi hiyo na kusema kuwa kuna wazee wengi ambao
wanaugonjwa wa macho.
Alisema kupitia kwao wanaweza kujitokeza kundi jengine hivyo
kulitaka shirika hilo kuwa na moyo wa kusaidia na kuwataka wengine kuiga mfano
huo.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mwanasha Tumbo, akimvisha miwani, Mwajuma Omari mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho uliofanywa na Taasisi ya Medewell Charitable Health Centre kutoka Kibaha Mkoani Pwani .
No comments:
Post a Comment