Sunday, February 26, 2017

DC, KOROGWE APIGA MARUFUKU UPIGAJI GONGO, MAJIMAREFU AWA MBOGO



Korogwe, MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Robarts Gabriel, amepiga marufuku upikaji wa pombe haramu ya Gongo na kutoa agizo kwa askari mgambo kuwakamata wapigaji na wanywaji.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana kijiji cha Mgilla Tarafa ya Bungu  ulioitishwa na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stevin Ngonyani maarufu  (Majimarefu), Gabriel alisema ni marufuku upigaji wa Gongo katika Wilaya yake.
Alisema ofisi yake ikiongozwa na yeye mwenyewe atapita kijiji kimoja kimoja kusaka nyumba zinazipikwa gongo na kuiharibu mitambo ikiwa na pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
“Natoa agizo kwa askari wa mgambo kila kijiji kuhakikisha wanawafikisha katika vyombo vya sheria wapikaji wa gongo na mitambo yake ifikishwe katika ofisi yangu kama kielelezo” alisema Gabriel na kuongeza
“Zoezi hili litaenda sambamba na wakulima wa bangi ambao majina yao niko nayo, watu wamebadilisha kilimo cha mazao na kulima bangi na nitawakamata” alisema
Gabriel aliwataka wananchi hao kutayarisha mashamba kwa ajili ya msimu wa kilimo cha mahindi na mihogo kipindi hiki cha kuanza kwa mvua na kuacha kuuza mashamba.
Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stivin Ngonyani, aliwatahadharisha wenyeviti wa vitongoji na vijijini awamu ya tatu ya Tasaf kuandikisha walengwa na kuacha kuandikisha majina kwa kujuana.
Alisema kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakiandikisha majina kwa kujuana na ambao wanastahiki kuachwa na kusema kuwa awamu hii atakuwa nao sambamba.
‘Awamu hii ya tatu ya  Tasaf nitakula sahani moja na watendaji na wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao watabainika kuandikisha majina kw amisingi ya kujuana na kuacha wanastahiki” alisema Majimarefu
Aliwataka wananchi hao kutoa taarifa katika ofisi yake ya Mbunge kama kutatokea ukiukwaji wowote wa kuorodhesha majina na kuachwa wanastahiki.



Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stevin Ngonyani CCM (Majimarefu) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Magundi Tarafa ya Bungu jimbo la Korogwe Vijijini wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wanachi jimboni humo juzi.






Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini CCM, Stivin Ngonyani (Majimarefu) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kwashemshi Tarafa ya Bungu kusikiliza kero za wananchi jimboni humo juzi.

No comments:

Post a Comment