Tanga, KOCHA Mkuu wa timu ya Sahare FC
inayoshiriki ligi daraja la nne ngazi ya Mkoa, Joseph Lazaro, amesema timu yake
kupata bao la kusawazisha dakika za nyongeza dhidi ya Korogwe FC ni miujiza ya
Mungu.
Akizungumza na vyombo
vya habari mara baada ya kumalizika mchezo huo, Lazaro alisema alivyoichukulia
timu hiyo ni tofauti walivyouanza mchezo.
Alisema alivyojua timu za mashamba haziwezi kufua dafu kwa
timu za mjini lakini kwa timu ya Korogwe haikuwa hivyo bali kuanzia mwanzo wa
mchezo hadi kipenga cha mwisho walikuwa bora zaidi yao.
“Dah kwa kweli nilivyowachukulia wapinzani wetu ni tofauti na
ilivyokuwa imani yangu jogoo wa shamba hawiki mjini lakini kumbe sio hivyo
wametuendesha puta” alisema Lazaro na kuongeza
“Kipindi cha pili kidogo tulionyesha matumaini ya kutafuta
magoli lakini nao wenzetu walikuwa wakilinda goli, ila nisema goli lile la
kuwaswazisha dakia za nyongeza ni
miujiza ya Mungu
Amewataka wachezaji wake kujifunza kwa mchezo huo kwa kufanya
mazoezi kwa bidii ili kufanya vizuri katika michezo iliyoko mbele yao na kuweza kujiweka
nafasi nzuri.
Kwa upande wake, kocha wa Korogwe FC, Salim Juma Makame,
amewataka wachezaji wake kujilaumu kwa kushindwa kulinda goli na kuruhusu
Sahare kusawazisha dakika za nyongeza.
Alisema kwa mchezo huo atafanya mabadiliko madogo katika safu
ya ulinzi na ushambuliaji na kubadilisha mfumo wa uchezaji badala wa sasa wa
kupiga mipira mirefu.
“Dakika za majeruhi wachezaji wangu walikuwa hawaelewani
uwanjani na kucheza fyongo na kupelekea kuruhusu goli dakia za mwisho” alisema
Makame
Aliwataka wachezaji wake kusahau matokeo hayo na kuangalia mchezo ambao
uko mbele yao na kuweza kufanya vizuri mwanzo mwisho.
Kiungo wa Sahare FC, Ali Salim (chini) akigombea mpra na mchezaji wa Korogwe FC, Martin Thomas wakati wa mchezo ligi daraja la nne ngazi ya Mkoa uwanja wa Mkwakwani juzi, Timu hizo zilitoka suluhu kwa kufungana bao 1, 1.
Mshambuliaji wa Korogwe FC (8), James Semi akigombea mpira na kiungo wa Sahare FC, Abdull Mgaya wakati wa mchezo ligi daraja la nne ngazi ya Mkoa uwanja wa Mkwakwani juzi, Timu hizo zilitoka suluhu kwa kufungana bao 1 , 1.
No comments:
Post a Comment