Monday, February 13, 2017

MWANAMKE MWENYE UZITO MKUBWA DUNIANI ATUA INDIA KWA UPASUAJI

Eman Ahmed Abd El Aty mwenye ana umri wa miaka 36Eman AhmedMwanamke raia wa Misri, ambaye inasadikika kwamba ndiye mwenye uzani wa juu zaidi duniani, amewasili mjini Mumbai nchini India kufanyiwa upasuaji.
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye umri wa miaka 36 ana uzani wa kilo 500 na anahitaji kufanyiwa upasuaji kumsaidia kupunguza uzani wake.
Safari hiyo ya Jumamosi ilikuwa mara yake ya kwanza kwake kuondoka nyumbani katika kipindi cha miaka 25.
"Eman aliyesafiri kwa ndege ya EgyptAir aliwasili katika uwanja wa ndege wa Mumbai majira ya saa kumi alfajiri na akafika hospitalini Saifee mwendo was aa kumi na mbili alfajiri. Kitanda maalum alicholalia kiliinulia, yeye akiwa bado kitandani, kwa kutumia kreni," madaktari walisema.

No comments:

Post a Comment