Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon, Christian Bassogog
amechaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika iliyomalizika nchini Gabon mwaka huu 2017.
Mchezaji huyo
amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya Cameroon kuweza kutwaa Kombe la
AFCON, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri kwenye mchezo wa fainali
ambao ulipigwa katika dimba l'Amitie mjini Libreville na kutajwa
kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano na Kamati ya Ufundi ya CAF na kikundi
cha Watathmini.
Orodha ya waxchezaji wengine waliofanya vizuri
katika michuano hiyo ni Mchezaji Bora wa Benjamin MOUKANDJO
(Cameroon), Tuzo ya Fair Play - Misri, Mfungaji Bora-Junior KABANANGA
(DRC) Mabao 3, Kikosi cha Mashindano cha CAF - Kipa Fabrice ONDOA
(Cameroon),Mabeki- Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Misri),
Michael NGADEU (Cameroon)
Viungo-Charles KABORE (Burkina Faso),
Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU
(Ghana), Mohamed SALAH (Misri) .
No comments:
Post a Comment