Monday, February 13, 2017

MKALIMANI ALIEPOTOSHA MANENO YA MTALII AIBUKA, AOMBA RADHI

Mkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtaliiMkalimani anayedaiwa kutafsiri maneno yasiyo sahihi kutoka kwa mmoja wa watalii aliyetembea hifadhi ya Ngorongoro, hatimaye ameibuka na kuomba radhi kutokana na video hiyo iliyosambaa kwa madai kuwa alikuwa katika mazingira ya kufanya utani.
Awali mkalimani huyo anayeitwa Simon Sirikwa aliwekwa chini ya ulinzi kutokana kile kilichokuwakinatafsiriwa kudaiwa kuwa kilikuwa kinapotosha uhalisia wa maneno yaliyokuwa yakizungumzwa na mtalii aliyekuwa akisifia kile alichokiona baada ya kutembelea eneo hilo la utalii.
Hata hivyo katika video mpya aliyoitoa akiwa na mtalii yule yule aliyeonekana katika video ya kwanza, amesikika akizungumza kwa lugha ya Kiswahili akiomba radhi kwa kile alichokuwa amezungumza kwenye video ya awali.
"Kama mlivyoona video yangu niliyopitisha mimi ni tour guide kwa zaidi ya miaka kumi sasa, siwezi kuichafua hii nchi hata kidogo, hata aliyetoa hiyo video kwenye Facebook, kwenda kwenye Whatsapp na kuisambaza kwenye makundi ya kijamii atakuwa amekosea," amesema Sirikwa.
"Lakini ilikuwa ni comedy, ilikuwa ni utani, na najua kuna watu wamekwazika, ila naomba samahani kwa waliokwazika, ila kwa mafansi wangu, wafuasi wangu endeleeni kupata burudani, ila mfahamu sijafanya hichi kitu kwa serious wala sikuwa na makusudio yoyote mabaya, asanteni."
Baadhi ya watu wanaomfahamu Sirikwa walipohojiwa na BBC wamemuelezea alivyo mtu wa utani na kwamba anajulikana kwa jina la utani kama Mpondamali.
BBC

No comments:

Post a Comment