Tanga, MEYA wa jiji la Tanga, Mustapha
Mhina, amepiga marufuku uvaaji wa suruali aina ya jeanzi wakati wa vikao vya
baraza na kuwataka kuheshimu vyenginevyo kanuni za baraza kwa kuwatoa nje.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani jana, Mhina
alisema ni marufuku kuvaa suruali aina ya jeanzi pamoja na mavazi mengine
ambayo hayana staha ndani ya baraza.
Alisema kwa muda mrefu amekuwa akioona tabia hiyo na
kuivumilia jambo ambalo amelichunguza hakuna mabadiliko hivyo kanuni za baraza
zitafanya kazi bila ya kuonea mtu hutuma wala sura.
“Waheshimiwa madiwani mwisho leo kumuona diwani amevaa
suruali aina ya jeanzi au mavazi ambayo hayana staha si kwa wanawake wala
wanaume” alisema Mhina na kuongeza
“Hiki ni chombo kinatakiwa kuheshimiwa na kila mjumbe wa
baraza hili natoa angalizo mapema kikao kijacho kabla ya kuanza kwa baraza
nafanya ukaguzi” alisema
Alisema kuanzia sasa atakuwa mkali kwa kila jambo ambalo
ataliona haliko sawa ndani ya baraza ikiwemo kufika kwa wakati ndani ya baraza
na utoro ambao hautakuwa na taarifa.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Maweni , Joseph Collivas
(CCM) amewataka wajumbe wa baraza la madiwani kutoa kero za wananchi katika
maeneo yao na kuyapatia ufumbuzi wa haraka.
Alisema kuna changamoto nyingi katika maeneo ambayo madiwani
wanawakilisha lakini hadi muda wa sasa hakuna hatua zozote ambazo zimepatiwa
ufumbuzi ikiwemo mrefeji wa maji eneo la stendi kuu ya mabasi ya Kande ambayo
hayana uelekeo.
“Madiwani wenzangu hebu tujadilini kero za wananchi ambao
wametuchagua na kuyapatia ufumbuzi, kila mmoja kwake kuna kero kama sio dampo
kuna migogoro iwe ya mipaka au ya viwanja” alisema
Aliwataka madiwnai hao kuhakikisha wanavitumia vikao hivyo
kwa manufaa kwa wananchi bila kuangalia chama kwa madai kuwa kinachotakiwa ni
maendeleo ya wananchi.
Mwisho
.Meya wa jiji la Tanga, Mustafa Mhina (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani
No comments:
Post a Comment