Thursday, February 9, 2017

WATU WASIOJULIKANA WAVUNJA NYUMBA USIKU, KANGE TANGA



Tanga, SIKU tano baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo, William Lukuvi kufanya ziara Mkoani Tanga, watu wasiojulikana wamevunja nyumba nne usiku wa kuamkia jana.
Watu hao wanaosadikika kuwa zaidi ya kumi walitumia nyundo na sururu na kufanikiwa kuvunja milango ya nyumba na kuzidondosha chini yakiwemo maboma mawili zilizoko mtaa wa Kichangani kata  Maweni.
Mhanga wa tukio hilo, Spora Raphael alisema walifika watu zaidi ya kumi kumtaka afungue mlango na kugoma ndipo walipotumia nyundo kuvunja mlango na kupita ndani.
Alisema watu hao waliokuwa na mapanga na nyundo walimtaka kuhama katika nyumba hiyo na kulalamika kuwa yuko na watoto peke yao na hajui angenda wapi ndipo walipomsamehe na kundi hilo  kuondoka.
Kwa upande wake Diwani kata ya Maweni Joseph Collivas, alisema eneo hilo liko na mgogoro wa muda mrefu na kutoa tuhuma kuwa mipango miji wanaulea.
Amesema wakazi wa eneo hilo walipimiwa viwanja hivyo ikiwa ni fidia ya viwanja vya Saru Magaoni ambao walitakiw akupisha ujenzi wa reli kuelekea bandari mpya ya Mwambani.






No comments:

Post a Comment