Tanga, KOCHA Mkuu wa timu ya Kwamdolwa FC
ya Korogwe Tanga inayoshiriki ligi daraja la nne ngazi ya Mkoa, Dankan Mwamba
ameitupia lawama timu yake kwa kukubali
kipigo cha mabao 3, 1 kutoka kwa timu ya Majengo FC ya Tanga.
Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo uwanja wa
Mkwakwani jana, Dankan, alisema wachezaji wake walicheza mchezo mbovu na kudai
kuwa sivyo alivyowafundisha kucheza.
Alisema kipigo hicho ni lawama kuanzia kipa hadi mchezaji wa
mwisho na kuwataka wachezaji wake kubadilika haraka vyenginevyo kikosi chake
atakipangua upya.
“Sijafurahishwa na uchezaji wa wachezaji wangu ni tofauti
kabisa na mafundisho ambayo nimekuwa nikiwaelekeza wakati wa mazoezi” alisema
Dankan na kuongeza
“Wakati wa mazoezi kila mmoja ukimuangalia unamuona bora na
kushindwa nani kumuanzisha, lakini wakati wa mechi uwanjani ni tofauti kabisa
na kubaki kuumwa na kichwa” alisema
Aliwataka wachezaji wake kukichukulia kipigo hicho kama
changamoto ya kupata matokea mazuri katika michezo iliyoko mbele yao na kusema
kuwa wanarejea Korogwe na kutokuwa na lakuwambia washabiki wa timu yake.
Kwa upande wake kocha wa Majengo FC ya mjini Tanga, Shaban
Bakari, amesema ushindi huo wa mabao 3 umewatia mori wachezaji wake wakiwemo
wakufunzi wa timu hiyo.
“Kila siku hufurahi
kupata pointi tatu lakini leo nimepata pointi tatu na magoli matatu
jambo ambalo linanifanya niweze kutembea kifua mbele mitaa” alisema Bakari
Aliwataka wachezaji wake kutobweteka na ushindi huo badala
yake kuongeza kasi ya mazoezi na bidii uwanjani ili kuweza kupata matokeo
mazuri mfululizo.
Mwisho
Mchezaji wa Kwamdolwa FC, Ali Vote (5) akigombea mpira na mchezaji wa Majengo FC wakati wa mchezo ligi daraja la nne ngazi ya Mkoa uwanja wa Mkwakwani juzi, Majengo iliibuika na ushindi wa mabao 3, 1.
No comments:
Post a Comment