Monday, February 6, 2017

KOCHA WA PANONE ADAI KIPIGO KITAKATIFU NI MZIMU WA KOCHA ALIETIMULIWA



Tanga, KOCHA Mkuu wa timu ya Panone FC ya Moshi  inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania Bara, Pitter Mtega amesema kipigo walichoshushiwa na Mgambo JKT cha mabao 4 ni mzimu wa kocha alietimuliwa Jumanne Mtambi.
Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo uwanja wa Mkwakwani juzi, Mtega alisema itachukua muda timu hiyo kukaa sawa hadi mzimu wote wa kocha alietimuliwa utakaposambaratika.
Alisema ni aibu kufungwa mabao mengi bila kuambulia goli moja na kudai kuwa anaamini kuwa timu hiyo itafanya vizuri watakaporejea Moshi hivyo kuwataka washabiki wake kuwa wavumilivu.
“Kipigo tulichopokea silaumiki kila mtu anajua kuwa ni mzimu wa kocha alitimuliwa kwa matokeo yake mabaya kila mechi hivyo kwa sasa ndio naisuka na nina imani kuwa tutasimama pazuri” alisem Mtega
Aliwataka wachezaji wake kutuliza akili na kusahau ya kocha alietangulia badala yake kufanya  mazoezi ya nguvu kwa kuamini kuwa safari bado inaanza.
Kwa upande wake kocha Mgambo JKT, Abdi Said, amesema amepata faraja kwa kupata ushindi mnono wa mabao 4 ikiwa ni mchezo wake wa kwanza toka aichukue timu hiyo kutoka kwa mtangulizi wake.
Alisema wakati wa mchezo aliwangalia wachezaji wake maelekezo ambayo aliyatoka wakati wa mazoezi hadi wanaingia uwanjani kama watayafuata na uzuri wake hawakumuangusha.
Alisema yuko na imani ya kufanya vizuri zaidi kufuatia maelekezo yake kufuatwa na wachezaji na kuwataka ushirikiano pamoja na washabiki uwanjani na nje ya uwanja.
“Huu ni mchezo wangu wa kwanza na leo nimepata magoli manne bila kuruhusu goli kuingia langoni mwangu, niwambie wapenzi na washabiki wa mpira Tanga heshima iliyotoweka itarudi” alisema Said
Aliwataka wana Tanga kumpa ushirikiano ili kuhakikisha soka la Tanga linarudi kwa kuzipandisha timu zote ambazo zilikuwa ligi kuu Tanzania Bara.
                                             



 Kiungo wa timu ya Panone FC ,Adam Dunde akiwania mpira na mchezaji wa Mgambo JKT, Bashiru Mohammed wakati wa mchezo ligi daraja la kwanza Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Mgambo JKT iliibuka kwa ushindi wa mabao 4, 0.
Mchezaji wa Mgambo JKT, wakifukuzia mpira na wachezaji wa Panone FC ya mjini Moshi wakati w amchezo ligi daraja la kwanza Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Mgambo JKT iliibuka na ushindi wa mabao 4  , 0.
Mchezaji wa Mgambo JKT, Athumani Ally, akipiga kichwa katikati ya wachezaji wa Panone FC,  kuokoa mpira langoni kwake wakati wa mchezo ligi daraja  kwanza  Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Mgambo JKT iliibuka na ushindi wa magoli 4  ,  0.

No comments:

Post a Comment