Sunday, February 12, 2017

JKT RUVU WAWALAMBISHA MBAO MABAO 2 BILA HURUMA

 Timu ya JKT Ruvu, imeitandika timu ya Mbao mabao 2, 0 wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom) mchezo uliochezwa  Uwanja wa Mkwakwani.
Akizungumza mara baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo huo, Kocha wa Mbao, Etienne Ndayiragije, alisema timu yake haikucheza vizuri na JKT walistahili ushindi  hivyo wanarudi kwao kutafakari kipigo hicho cha ugenini.
Kwa upande wake, Kocha wa JKT Ruvu, Bakari Shime, alisema walistahili ushindi kwa madai kuwa vijana wake walicheza vizuri zaidi ya wapinzani wao.


No comments:

Post a Comment