Saturday, February 4, 2017

DONALD TRUMP APATA PIGO LA KWANZA ZUIO LA WAISLAMU MAREKANI

Kampuni ya ndege ya Qatar AirlineIdara ya forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.
Shirika la ndege la Ghuba, Qatar Airways, lilisema litaanza kupakia abiria haraka.
Raia wa mataifa 7 ya Waislamu sasa kuingia Marekani
Hatua hiyo inafuata saa tu baada ya jaji wa mahakama ya taifa ya Marekani, kuzuia amri hiyo ya Rais Trump kwa muda.
Mahakama iliamua kuwa hatua ya rais ilivunja katiba, ambayo inakataza dini moja kupendelewa kushinda nyengine.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment