Saturday, February 11, 2017

KUTOKA UWANJA WA TAIFA, SIMBA VS PRISON



Dk 23, Asukile anaingia vizuri, anamtoka kipa Agyei lakini mpira unaokolewa na kuwa kona ya kwanza ya Prisons lakini Agyei anadaka kwa ufundi hapa
Dk 20, Simba wanapata kona ya pili, inachongwa hapa na Mavugo anautupia mpira wavuni lakini kabla Liuzio alifanya faulo
GOOOOOOO DK 18, krosi ya Bukungu inagongwa na kumkuta Liuzio, anaweka kifuani na kuandika bao la kwanza kwa Simba leo na la kwanza kwake katika Ligi kuu Bara
Dk 17, kona ya kwanza ya mchezo wanapata Simba baada Prisons kuokoa

Dk 15, krosi nzuri ya Ajibu, Mavugo anaiwahi ndani ya 12 lakini mwamuzi anasema amecheza mashambi
Dk 12, Asukile anapiga kichwa hapa lakini hakulenga lango na inakuwa goal kick
Dk 10, Liuzio anaingia kwa kasi anatoa krosi hapa lakini Mpalile na wenzake wanaokoa hapa


Dk 7 sasa, mpira upo katikati zaidi huku Prisons wakiendelea kuwa nyuma zaidi wakilinda
Dk 5 sasa, Simba wanaonekana kuhamia kwenye lango la Prisons, lakini walinzi wa Prisons wanaonekana bado wako makini
Dk 3 anamchambua Mpalile, anaachia shuti lakini si kali na halikulenga lango
Dk 2, Ajibu anapokea pasi nzuri ya Ndemla lakini kipa anatokea na kuokoa vizuriii kabisa
Dk ya 1, Simba wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Prisons lakini kipa Aron Kalambo anadaka kwa ulaini

No comments:

Post a Comment