Uber kutengeza magari yanayoruka
Muhandisi wa zamani
wa shirika la maswala ya angani Nasa ameajiriwa na kampuni ya teksi
Uber kusaidia katika utafiti wake wa kutengeza magari yanayoruka.
Mark Moore anajiunga na Uber kama mkurugenzi wa uhandisi wa angani.Lengo la Uber katika kutengeza magari yanayoruka lilikuja baada ya mwezi Oktoba ambapo maswala ya kupaa na kutua yalijadiliwa.
Uber tayari inawekeza katika magari ya kujiendesha ikishirikiana na kampuni ya Volvo na Daimler.
Katika mipango yake Uber imesema kuwa katika mahitaji ya angani ,kampuni hiyo ina uwezo wa kuimarisha uchukuzi wa mijini na kuwapatia wateja wake muda wanaopoteza kila siku wanaposafiri.
Alisema kuwa mpango wa kutengeza vitu vinavyopaa kielektroniki ni mpango muhimu wa kiteknolojia wa ndege na kuongezea kwamba kitu kinachozuia kuanza kwa mpango huo ni betri zitakazotumika.
Kampuni ya kutengeza magari ya ya Aeromobil kutoka nchini Slovakia ni miongoni mwa kampuni ambazo zina mpango wa kutengeza gari la kuruka ambayo inatarajiwa kuingia katika soko mwaka huu.
No comments:
Post a Comment