Monday, January 26, 2015

KIJANA AMKABA BABU YAKE NA MUMUUA

Baada ya kumtaka mjukuu wake atafute kazi mwenyewe afanya maamuzi haya.

handcuff-stposed1eMzazi au mlezi ni watu ambao wanategemewa na watoto wao katika ushauri hasa pale anapotaka kufanya jambo na wengi wamekuwa na mafanikio kwa kufata ushauri huo, lakini hii imekuwa tofauti kwa Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17, ambae anashikiliwa na Polisi nchini Japan kwa tuhuma za kumuua Babu yake mwenye umri wa miaka 73, baada ya kumkaba kwa kutumia Blangeti.
Uchunguzi unaonyesha kuwa awali uliibuka ubishani katika ya Polisi na Kijana huyo ambae haikujulikana kama ni mjukuu wake, na baada ya mahijiano mtuhumiwa huyo alikiri kumuua babu yake kwa kumnyonga hadi kufa baada ya kushikwa na hasira alipomwambia akatafute kazi.
 Mwili wa mzee huyo ulikutwa ukiwa umefungwa katika blangeti ndani ya chumba chake.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment