Wednesday, January 28, 2015

MATOKEO YA MTANANGE WA LIGI KUU VODACOM HAYA HAPA

Matokeo ya Mechi za Simba Vs Mbeya City, TP Mazembe Vs Azam FC yote hapa

soccer-start-and-restart-of-play
Mechi kati ya timu ya Simba SC na Mbeya City imemaliza muda mfupi uliopita, Simba wamejikutawakikubali kichapo cha goli 2-1 katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Hamad Kibopile na Yusuph Abdallah aliyefunga kwa njia ya penalti, wakati goli la Simba limefungwa na Ibrahim Hajib ‘Mido’.
Hata hivyo dakika ya mwisho ya mchezo, Masoud Nassor ‘Cholo’ amekosa mkwaju wa penalti baada ya beki Yusuph kumfanyia madhambi Jonas Mkude katika eneo la hatari.
Hiki ni kipigo cha pili kwa Simba ndani ya uwanja wa Taifa, December 26 mwaka jana walifungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Mechi kati ya timu ya TP Mazembe ya Congo na Azam FC ambayo imemalizika pia muda mfupi uliopita katika Uwanja wa timu ya TP Mazembe ambapo wenyeji hao wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment