Wednesday, January 28, 2015

MCHUNGAJI AINGIA MATATANI AFRIKA KUSINI

Utata wa video ya Mchungaji iliyozagaa mitandaoni ikionyesha akiwa bila nguo Afrika Kusini!

PasortMchungaji maarufu Afrika Kusini Sthembiso Zondo ambae huwa anatoa mahubiri yake kwa njia ya Redio nchini humo, ratiba ya kurushwa kwa mahubiri yake imesimamishwa kurushwa hewani  baada ya kuvuja video inayomuonyesha akizungumza kwenye simu huku akiwa hajavaa nguo yoyote.
.
Mchungaji Sthembiso Zondo
Shirika la utangazaji la Afrika Kusini (SABC) limetoa amri ya kusimamishwa kwa Kipindi cha mchungaji huyo hadi itakapotangazwa tena, maamuzi yaliyotolewa baada ya video inayomuonyesha Mchungaji Zondo akiwa hajavaa nguo iliyowekwa kwenye mitandao, video hiyo inaonyesha kuwa ilirekodiwa na mwanamke aliyekuwa amevaa skirt ya pink lakini hakuweza kutambulika.
Taarifa zinasema kuwa Zondo aliomba radhi kutokana na kuvuja kwa video hiyo, japo kulikuwa na mvutano pia wengine wakilaumu aliyevujisha video hiyo huku wengine wakimfata mchungaji huyo ajieleze kuhusu video hiyo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment