Wednesday, January 28, 2015

MANNY PACQUAIO NA FLIYD MAYWEATHER USO USO UWANJANI

Manny Pacquaio na Floyd Mayweather uso kwa uso Marekani.

big 6

Mabondia wawili nyota Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hapo jana walikutana uso kwa uso ikiwa ni mara ya kwanza kukutana katika kipindi hiki ambacho pambano lao limekuwa likitajwa sana .
Mabondia hao walikutana kwenye uwanja wa American Airlines Arena ambako walikuwa wakitazama mchezo wa ligi ya mpira wa kikapu ya NBA kati ya Miami Heat na Milwaukee Bucks .
Pacquaio alihudhuria mchezo huo akiwa mgeni wa kocha wa Miami Heat Erik Spoelstra na Floyd kwa upande wake amezoeleka kama shabiki mkubwa wa Miami na amekuwa akihudhuria michezo mingi ya timu hiyo .
Mayweather na Pacman wakionekana pamoja kwenye mchezo wa NBA nchini Marekani .
Mayweather na Pacman wakionekana pamoja kwenye mchezo wa NBA nchini Marekani .
Mabondia hao walionekana wakizungumza kwa kifupi kabla ya kupeana mkono na kuagana huku kila mmoja akienda kivyake .
Hivi karibuni mashabiki wa masumbwi wamekuwa wakizungumza kuhusu pambano la mabondia hao wawili na kumekuwa na mazungumzo ambayo yanaendelea japo hayajaweza kufikia hatua yoyote nzuri .
Hapa walionekana kama wanabadilishana namba za simu .
Hapa walionekana kama wanabadilishana namba za simu .

Hapa walipeana mikono na kuagana
Hapa walipeana mikono na kuagana

big fight

No comments:

Post a Comment