Wednesday, January 28, 2015

MAMA MTOTO ALIEKUWA AKINGILIWA KIMWILI ANENA

Mtoto aliyekuwa akiingiliwa kimwili

images
Hekaheka ya leo January 28 inahusu mtoto wa kiume ambae alikuwa akiingiliwa kimwili kwa nguvu na vijana wawili ambao walikuwa wakimziba mdomo kwa kutumia nguo na kumtishia kwa kisu.
Mama wa mtoto huyo amesema aligundua tukio hilo wakati anafua nguo za ndani za mtoto huyo na kumueleza baba yake na alipomuuliza alisema kuna vijana wawili mtaani kwao wanamfanyia mchezo huo na alishindwa kusema kwa kuwa wamekuwa wakimtishia kumchoma kisu tumboni endapo atasema kwa mtu yoyote.
Wazazi hao wakaripoti Polisi katika kituo cha Gongo la Mboto na kupewa PF3 na kumpeleka Hospitali ya Amana na baada ya vipimo Daktari aliwaambia inaonyesha amekuwa akifanyiwa kitendo hicho kwa muda mrefu, ndipo walipoanza kuwatafuta kwa kushirikiana na wananchi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote wawili ambao mpaka sasa wako katika kituo cha Polisi cha Sitaki Shari.
Mwalimu wa Shule iliyoko maeneo hayo amesema kuwa Video Game za Play Station zilizoko maeneo hayo ndio chanzo cha kutokea matendo kama hayo na kuwafanya watoto wengi kutoroka darasani na kujiunga na vijana wa mtaani wanaojificha katika Bonde la Mto Msimbazi na kufanya vitendo viovu.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment