Tuesday, January 27, 2015

WASANII MORO WAPASUA JIPU

wasanii moro wapasua jipu

stamina_smJumanne ya January 27  kwenye 255 ya leo inahusu swala la wasanii kutoko Morogoro kupenda kukaa mkoani humo tofauti na wasanii wengine, ambapo msanii Stamina amezungumzia sababu ya yeye kupenda kukaa Moro ni kutokana na maisha kuwa rahisi ingawa mzunguko wa hela ni mdogo lakini maisha ni rahisi nani na ni mji uliotulia tofauti na Dar ambapo mzunguko wa hela ni mkubwa na maisha yako juu.
juxBaada ya Msanii Jux kwenda China kusoma inasemekana kuwa star huyo anafanya mambo mengine na sio shule peke yake, kwa kuwa hajawahi kuonyesha picha yoyote akiwa darasani au mazingira ya shule, msanii huyo amesema kuwa ni kweli anasoma na hawezi kupiga picha ili kuonyesha watu kwa kuwa mazingira ya shule hayaruhusu.
jkmStory ya mwisho kusikika inamhusu muigizaji Wema Sepetu baada ya gazeti moja kuandika kuwa anamdai shilingi milioni 10 aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz, Meneja wake Martin Kadinda amesema kuwa swala hilo limemchafua Wema kwa hiyo analitaka Gazeti hilo limuombe radhi na watoe tamko kuwa habari hiyo haikuwa ya kweli, akizungumzia swala la kuachana kwao amesema Wema hajampa taarifa zozote juu ya kuachana kwao ila hakuna hasara yoyote kwa kuwa kila mtu anaendelea na shughuli zake.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment