Thursday, January 29, 2015

SHEMEJI AVUNJA NDOA YA MDOGO WAKE

Sikia kisa hiki kinahusu shemeji anayelalamikiwa kuvunja ndoa ya mdogo wake.

DivorceNimekuwekea Hekaheka ya kumekuchablog ambayo inahusu mama anayemlalamikia shemeji yake aliyesababisha ndoa yake na mume wake kuvunjika.
Mama huyo amesema kuwa shemeji yake amekuwa na tabia ya kuingilia ndoa yake bila sababu yoyote na kusababisha kuwepo maneno yaliyopelekea mwanamke huyo kupewa talaka, baadeye aliamua kupeleka malalamiko yake kwenye chama cha kutetea wanawake na watoto Mwananyamala wakafanya kikao, mume alipoulizwa hakuweza kutoa sababu yoyote, shemeji yake huyo pia alipoulizwa alikana kuhusika kuvunja ndoa hiyo.
Mjumbe wa eneo hilo ambaye alipelekewa malalamiko hayo amesema alimfuata mwanaume huyo lakini alikataa kuzungumza, akamtupia lawama shemeji huyo kwa kuwa kabla hajaja kwenye nyumba hiyo hakukuwa na malalamiko yoyote, hata hivyo mwanamke huyo amesema hataondoka kwa mume wake na ameamua kupeleka suala hilo TAMWA.

No comments:

Post a Comment