Friday, January 30, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA , MAN YASHIKWA NA KIGUGUMIZI KWA BEKI HUYO

Huyu ndio beki ambaye Man United wamegoma kukanusha kutaka kumsajili

2501322500000578-2931379-image-a-51_1422537948921Dirisha la usajili barani ulaya limebakiza takribani masaa 48 kabla ya kufungwa, na kama ilivyo ada tetesi za usajili wa wachezaji tofauti zimezidi kushika kasi.
Klabu ya Manchester United ambayo imekuwa na udhaifu kwenye kikosi hasa kwenye maeneo ya kiungo na beki wa kati, leo hii Manchester United wameshindwa kukanusha taarifa kwamba wametuma ofa ya £37m kwa Borussia Dortmund na kuanza mazungumzo kwa ajili ya usajili wa beki  Mats Hummels. Inaaminika ikiwa usajili huo utafanikiwa basi beki wa Dinamo Kiev Aleksandar Dragovic atanunuliwa kurithi mikoba ya Hummels.
United wamekuwa wakihusishwa na usajili wa Mats Hummels tangu wakati wa dirisha la kiangazi lakini walikutana na kizingiti cha Dortmund kugoma kumuuza beki huyo mshindi wa kombe la dunia mwaka 2014, lakini sasa klabu hiyo ambayo ipo kwenye mkia wa msimamo wa Bundesliga inaonekana kuwa tayari kumuuza beki huyo ambaye pia alikuwa akihusishwa na kutakiwa na Arsenal.
Wakati huo huo mchezaji na nahodha msaidizi wa Man United Darren Fletcher anatarajiwa kujiunga na West Ham United kwa uhamisho wa bure na anategemewa kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa.

No comments:

Post a Comment