Tuesday, January 27, 2015

AJIOZESHA BAADA YA KUISHI MIAKA 40 YA UKAPERA

Mwanamke afikisha miaka 40 bila ndoa..hiki ndicho alichoamua!

alongMatukio ya wanawake kukata tamaa ya kuolewa kwa miaka ya sasa yameanza kuonekana ni ‘fashion’ huku wengi wakiona ni jambo la kawaida kuishi maisha ya peke yao.
Yasmin Eleby mwenyeji wa Houston, Marekani ameamua kufunga ndoa ya peke yake baada ya kufikisha miaka 40 bila kuona dalili yoyote ya kuolewa.
ele2
Eleby aliamua kufanya siku yake hiyo kuwa ya tukio muhimu kama ambavyo alikua akiota siku moja atakuja kuolewa na kufurahia siku hiyo ambapo aliwaalika baadhi ya ndugu zake na marafiki na kuamua kufanya sherehe hiyo katika ukumbi wa makumbusho wa Houston Museum.
Taratibu zote za arusi zilifuatwa na wageni waliohudhuria wakiwemo ndugu wa karibu na walimsapoti na kufurahia sherehe hiyo.
ele
Yasmin Eleby akiwa na wazazi wake siku ya harusi yake
Mwanamke huyo amepanga pia kwenda fungate ambapo atatembelea miji ya Laos, Cambodia, and Dubai.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment