Sunday, January 25, 2015

BODABODA WALALAMIKA UTITIRI WA KODI



 Tangakumekuchablog
Tanga,WAFANYABIASHARA wa pikipiki maarufu kama (Bodaboda) Tanga, wameitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na halmashauri ya jiji la Tanga kuwapunguzia wingi wa kodi vyenginevyo biashara hiyo inaweza kuwa ngumu kwao.

Wakizungumza katika kikao kilichowakutanisha, jeshi la polisi, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na halmashauri ya jiji la Tanga leo, wafanyabiashara hao wamesema kukuwa kwa sekta hiyo isiwe kafara kwa kuongezewa kodi.

Wamezitaja kodi hizo zikiwa ni shilingi  25,000 wanazotakiwa kulipa Mamlaka ya Mapato, kodi ya Insuarence,  kodi ya pikipiki (motavehecle), na kodi ya  fere instungsher pamoja na kodi ya maegesho ya pikipiki zao ambazo zote hizo ni vigumu kulipika kulingana na kipato chao.

“Waheshiwa meza kuu hamuoni kodi hizi kama munatubebesha wakati hatustahili kulipishwa wakati sisi ni wavuja jasho----kuna watu wako na miradi mingi na mikubwa lakini hawana utitiri wa kodi kama za kwetu” alisema Fadhili Mfaume

“Jambo ambalo kama Serikali haitoweza kulivalia njuga ni kuruhusu kodi za kuzuka kama hii ya maegesho----vijana wengi wametokana na matukio mabaya ya uvutaji bangi na uporaji na leo unamfukuza aende wapi” alisema
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodaboda na bajaj 

Wilaya ya Tanga, Daudy Bilaly, amewataka madereva wa pikipiki na bajaj kuwa na umoja na mshikamano miongoni mwao ili kuweza kuiendeleza sekta hiyo na kuwa ya mfano.

Alisema kuna baadhi ya maeneo madereva wa bajaj na pikipiki wamekuwa hawana uelewano jambo ambalo ni baya katika sekta hiyo na hivyo kuwataka kuwa kitu kimoja.

“Jamani sekta yetu kila siku inakuwa kwa kasi na imekuwa mkombozi kwa watu ambao hawana kazi----hii imewavuta pia watu ambao walikuwa waporaji na wavuta bangi na kuona huku ndiko kuliko na riziki ya halali” alisema Daudy

Aliwataka madereva hao kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na yoyote ambaye  ataonekana kutumiliwa na watu waovu na kutoa siri za umoja wao katika kukabiliana na matukio ya kihalifu aripiotiwe katika vyombo husika na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza katika kikao hicho, kamanda wa usalama barabarani Mkoa wa Tanga, Abdi Issango, aliwataka madereva wa pikipiki kuacha mtindo ulioibuka wa kupakiza abiria zaidi ya mmoja na kusema kuwa msako wa kukomesha tabia hiyo utaanza mara moja.

Alisema ndani ya msako huo atakamatwa abiria ambaye amepakizwa mshikaki na ambaye hakuvaa kofia ngumu (helment) na kumtoza faini ya papo kwa papo au mahakamani.

“Kila siku tumekuwa tukipiga kelele kukemea uvunjifu wa sheria za usalama barabarani lakini elimu hiyo huingia sikioni na kutokea sikio la pili----sasa dawa imeiva na tunaingia barabarani” alisema Issango

Aliwataka abiria kugoma kupakizwa mishakaki na kuhakikisha dereva anakuwa na kofia mbili na endapo amembaini kuwa amelewa kugoma  kwani lolote laweza kujitokeza mbele ya safari ikiwemo kuibiwa  au kumsababishia ajali.

                                            Mwisho

No comments:

Post a Comment