Huyu kaamua kuingia na shela la harusi mitaani…kisa ni wazazi wake!
Mwanamke mmoja nchini Misri ameamua kukatiza na gauni la arusi mitaani kupinga masimango anayokutana nayo kwa kuchelewa kuolewa.Samah Hamdi mwenye miaka 27 alifikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na kashfa kutoka kwa watu wanaomzunguka ikiwemo familia yake hasa mama yake mzazi ambao wamekua wakimsema kutokana na kutokua na mume mpaka sasa.
Hamdi
ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili alisema ameamua kutembea
hivyo mitaani na kamwe hawezi kuacha dhamira yake hiyo ikiwa kama
ishara ya kupinga mila na desturi inayowakandamiza wanawake wasioolewa.Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti,tangakumekuchablog

No comments:
Post a Comment