Ana miaka 9 tu! afanya maajabu kwenye mti huu huko Kenya.
Kenya
imekuwa ikiingia kwenye headline mara nyingi kutokana na kuwepo na
matukio mbalimbali ambapo safari hii wakazi wa Kararia Marakwet bado
wanajiuliza uwezekano wa Mvulana mwenye umri wa miaka 9, kuweza
kuurudisha mti katika hali yake ya kuoteshwa ambao ulikuwa umeanguka
chini na ulikuwa ukikatwa kuni miaka mitatu iliyopita kwa kuunyanyua
peke yake bila kusaidiwa na mtu yoyote .Richard Komen mzazi wa mwanafunzi huyo amesema mtoto wake amekuwa na tabia za kufanya matukio ya kushangaza tangu kuzaliwa kwake.
”Nimekuwa nikijaribu kuelewa alivyofanya, nilipomuuliza alisema aliunyanyua mara ya kwanza kisha akapumzika kidogo na kisha akauinua tena mara ya pili hapo ndipo mti huo ulirejelea uhai wake” alisema Komen.
Watoto waliokuwa eneo hilo wamesema mvulana huyo aliwaambia wasogee pembeni kwa sababu alitaka kurejesha mti huo kama ulivyokuwa umeoteshwa awali, huku Kina mama wa eneo hilo wakisema mti huo uliangushwa na upepo mkali msimu wa mvua mwaka 2011, na wamekuwa wakiutumia kwa kukata kuni kwa matumizi ya nyumbani.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment