Friday, January 30, 2015

LUIS FIGO NA URAIS WAFIFA

Figo katika harakati za kuusogelea Urais wa FIFA

1224
Wagombea wawili wa nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa FIFA, Luis Figo na Prince Ali Bin Al Hussein wametangaza kupita hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye uchaguzi huo .
Haua hiyo inahusisha kuteuliwa kwa kutiliwa saini na vyama vitano vya soka toka kwenye nchi wanachama wa fifa .
Mchezaji wa zamani wa Ureno na klabu za Sporting Lisbon, FC Barcelona, Real Madrid na Inter Milan, Luis Figo na Rais wa chama cha soka cha Jordan ambaye pia ni makamu wa rais wa FIFA,  Prince Ali Bin Al Hussein ni moja kati ya watu sita ambao hadi sasa wametangaza dhamira ya wazi ya kuingia kwenye mbio hizo za kuwania urais wa FIFA.
Luis Figo amekidhi moja ya vigezo muhimu vya kugombea urais wa Fifa baada ya kuidhinishwa na vyama vitano vya soka toka barani ulaya .
Luis Figo amekidhi moja ya vigezo muhimu vya kugombea urais wa FIFA baada ya kuidhinishwa na vyama vitano vya soka toka barani Ulaya.
Moja ya vigezo vya kuingia kwenye mbio za urais wa FIFA ni kwa kila mgombea kuwasilisha barua zilizotiwa saini na vyama vya soka vya mataifa angalau matano na mpaka kufikia hii leo (Alhamisi) tayari Figo na mtoto wa Mfalme wa Jordan walikuwa wametimiza kigezo hicho.
Inaaminika kua vyama vya soka vya Denmark, Ureno, Montenegro, Macedonia, Luxembourg na Poland ndio vyama vilivyompitisha Figo.
Kwa upande wake Prince Ali alithibitisha kupitia kwenye kigezo hicho ambapo alitumia ukurasa wake binafasi wa Twitter kuwaeleza watu wake kuwa tayari amepata saini za vyama vitano.
Prince Ali Bin Al Hussein naye amepata idhini toka kwa vyama vitano vya soka .
Prince Ali Bin Al Hussein.
Hadi sasa ukiachilia mbali Figo na Pirnce Ali wagombea wengine waliojitokeza ni mchezaji wa zamani wa Ufaransa  David Ginola, kiongozi wa zamani wa FIFA Jerome Champagne, rais wa chama cha soka cha Uholanzi, Michel Van Praag pamoja na rais wa sasa, Sepp Blatter.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment