Tuesday, January 27, 2015

POLISI WAWATAWANYA WAFUASI WA CUF KWA MABOMU JANA

Mabomu ya machozi yatumika kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Wananchi CUF 

wafuasi+cuf 22
Kituo cha ITV kimeripoti kuwa Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Wananchi CUF, waliokuwa wanaenda kushiriki katika mkutano wa kuwa kumbuka wanachama wenzao waliouwawa huko Zanzibar mwaka 2001,  na kutumia nguvu kubwa kuwatawanya Waandishi wa Habari, ambapo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Pro. Ibrahim Lipumba na viongozi wengine walipigwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Hali hiyo ilianza katika Ofisi  za CUF Temeke baaada ya Pro. Lipumba kuwatangazia wafuasi hao kuwa, hakutakuwa na maandamano ya kwenda katika viwanja vya Mbagala Zakem na badala yake atakwenda mwenyewe kuwatangazia wananchi ambao tayari walikuwa wameanza kukusanyika katika eneo hilo la mkutano.
Wameiweka kwa makusudu kwasababu wanahitaji kuuwa watu wanahitaji watu wanajua kabisa kwamba kuna maandamano, Polisi wamezuia maandamano wanatupa taarifa wakati viongozi hawawezi kuipata taarifa hiyo, hakuna muda wa kuweza kuwasiliana na wananchi, kwa hiyo hili ni jambo lililofanywa kwa makusudi wala sio kwa bahati mbaya, kwa hiyo nawaomba nyie muweze kutulia kuweza kurudi kwenye shughuli zenu mimi nakwenda viwanja vya zakim kwasababu watu hawana taarifa watu wamekwenda kwenye viwanja vya mkutano hawana taarifa kama maandamano haya na mkutano wao umezuiliwa”–Alisema Pro. Lipumba
Hata hivyo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuyadhibiti maandamano hayo yaliyoleta tafrani kubwa kwa wananchi wa eneo hilo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment