Wednesday, January 28, 2015

ALOTELLI AANDAMWA NA MZIMU LIVERPOOL

Balotelli abebeshwa lawama za kufungwa kwa Liverpool.

ivanovic

Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli amebebshwa lawama za kipigo ambacho Liverpool ilikipata usiku wa jana katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Capitol 1 baada ya kushindwa kumkaba mfungaji wa bao pekee la Chelsea Branislav Ivanovic .
Chelsea ilishinda baada ya beki huyo raia wa Serbia Branislav Ivanovic kufunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Willian.
Balotelli alionekana kusimama nyuma ya Ivanovic akiwa anakabiliana naye ili amzuie asifunge bao wakati timu hizo zikiwa hazijafungana ndani ya muda wa nyingeza.
Wachezaji wa Liverpool wakijipanga mbele ya Branislav Ivanovic  kumzuia asifunge .
Wachezaji wa Liverpool wakijipanga mbele ya Branislav Ivanovic kumzuia asifunge .

Branislav Ivanovic akimkwepa Baloteli na kuzunguka nyuma yake kwenda kufunga .
Branislav Ivanovic akimkwepa Baloteli na kuzunguka nyuma yake kwenda kufunga .
Hata hivyo Ivanovic alimzunguka Balotelli na kumuacha ameduwaa ambapo alifunga bao kwa kichwa na lilitosha kuwapeleka Chelsea kwenye hatua ya fainali ya michuano hiyo .
Balotelli bado anaendelea kuandamwa na majanga akiwa na Liverpool ambapo tangu mwanzoni mwa msimu amelazimika kuzoea kutupiwa lawama hasa kutokana na kushindwa kufunga mabao hali ambayo imeonyesha kuwakera mashabiki wa Liverpool .
Wachezaji wa Liverpool Steven Gerard na Lucas wakikaba eneo ambalo halina mchezaji yoyote wa Chelsea .
Wachezaji wa Liverpool Steven Gerard na Lucas wakikaba eneo ambalo halina mchezaji yoyote wa Chelsea .

Baloteli akasogea mbele kujaribu kumkaba Diego Costa .
Baloteli akasogea mbele kujaribu kumkaba Diego Costa .

Jordan Henderson asogea kumkaba Diego Costa .
Jordan Henderson asogea kumkaba Diego Costa .

Wakati mpira ulipopigwa Jordan Henderson akazubaa na Diego Costa akamkimbia na kusogea mbele zaidi .
Wakati mpira ulipopigwa Jordan Henderson akazubaa na Diego Costa akamkimbia na kusogea mbele zaidi .
Wachezaji wa Chelsea hususan Diego Costa walikuwa wajanja na walisogea na kuwapumbaza mabeki wa Liverpool hali iliyowafanya wamsahau Branislav Ivanovic ambaye aliishia kufunga bao rahisi akiwa hajakabwa na mtu yoyote .
Diego Costa kama picha zinavyoonyesha alisogea eneo la Balotelli na Baloteli akasahau kumkaba Ivanovic na badala yake kumtazama Costa ambaye alitumika kama chambo kumtengenezea Ivanovic nafasi .
Henderson akiachwa akiwa amebaki kwenye eneo la kushoto na Costa akasogea aliko Balotelli .
Henderson akiachwa akiwa amebaki kwenye eneo la kushoto na Costa akasogea aliko Balotelli .

Balotelli mwishowe aliamua kuruka na Diego Costa na kumuacha Ivanovic akiruka bila kuguswa wala kukabwa na kufunga bao la ushindi .
Balotelli mwishowe aliamua kuruka na Diego Costa na kumuacha Ivanovic akiruka bila kuguswa wala kukabwa na kufunga bao la ushindi .

No comments:

Post a Comment