Wednesday, January 28, 2015

KINARA WA KUSAFIRISHA MIHADARATI AKAMATWA KOROGWE



Kumekuchablog
Tanga,POLISI Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, wamemkamata kondakta wa basi, Abdalla Kayomba (37) ambaye anasadikiwa kuwa ndie msafirishaji mzoefu wa mihadharati aina ya mirungii kati ya Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Juma Ndaki, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa  leo saa 6 kwenye kizuizi cha polisi kijiji cha Chekelei Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe.

Alisema wakati wa kukamatwa kwake  kijana huyo alikutwa na kilo 35 za mirungi ambayo alikuwa ameificha chini ya uvungu wa lori na kuweka katika magunia mawili ya mkaa .

“Kwanza baada ya polisi kumuona tu walimuweka chini ya ulinzi kwani alikuwa akisakwa kwa udi na uvumba----wakati wa mahojiano alifichua siri na kueleza bayana kusafirisha kilo 35 za mirungi” alisema Ndaki na kuongeza

“Polisi walipoiona tu sura yake walimkwida na kumuweka chini ya ulinzi----nae hakufanya shida kwani alikuwa akijua kuwa anawindwa na sasa anahojiwa kutoa taarifa ili kuuzima mtandao wa usafirishaji mihadharati” alisema

Alisema wakati polisi wakifichua mirungi hiyo ambayo ilikuwa imefichwa katika magunia ya mkaa ilikuwa vigumu kuigundua lakini walipatwa na hofu baada ya kusikia harufu kali iliyoasghiria mirungi.

Katika hali nyengine, kaimu kamanda wa polisi aliwataka wananchi wanaoishi kandokando ya milima ya Usambara Wilayani Korogwe na Lushoto kutoa taarifa za watu wanaojishughulisha na kilimo cha bangi.

Alisema kilimo hicho kimekuwa kikishamiri katika Wilaya hizo na hivyo kutoa wito kwa wakulima waliobadilisha aina ya kilimo na badala yake kulima bangi kuwa msako wa kuwasaka uko karibu.

“Natoa wito kwa wakazi wanaoishi karibu na milima ambayo yunadhani kuna watu wamebadilisha aina ya kilimo na kulima bangi kuwafichua na kutupa taarifa----polisi imejipanga kufanya msako usiku na mchana” alisema Ndaki

Alisema tabia ya watu kulima bangi badala kilimo cha chakula kunaifadhaisha jamii kwani eneo hilo kila mwaka hukumbwa na njaa huku chanzo kikiwa ni wakulima kubadilisha kilimo.

                                       Mwisho

No comments:

Post a Comment