Pigo Chelsea! Hii ndio adhabu iliyomkuta Diego Costa leo hii
 Masaa
 takribani 24 kabla ya klabu ya Chelsea kuwakaribisha mabingwa watetezi 
wa Barclays Premier League Manchester City katika dimba lao la Stamford 
Bridge katika mchezo muhimu wa ligi kuu ya England – vijana wa Jose 
Mourinho wamepata pigo zito katika kikosi chao.

Mshambuliaji wao tegemeo ambaye 
ameshafunga magoli 17 kwenye ligi mpaka sasa, Diego Costa amefungiwa 
mechi 3 kwa kosa la kumkanyaga makusudi mchezaji wa Liverpool Emre Can.
Costa mwenye umri wa miaka 26 atakosa mechi ya wikendi dhidi ya Mancity pamoja na mechi dhidi ya Aston Villa na Everton.Shtaka hilo ambalo Costa alilikana linatokana na tukio lake alilofanya kwenye mchezo wa kombe la Capital One Cup ambapo Chelsea iliibuka kidedea.
Costa aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni millioni 32 ana mabao 17 katika mechi 19 za ligi ya Uingereza msimu huu.
 
No comments:
Post a Comment