Baada ya Whitney Houston kufariki kwa dawa za kulevya, vipi kuhusu hili la mwanaye?
Mtoto wa marehemu Whitney Houston, aitwaye Bobbi Kristina Brown amekutwa katika hali mbaya nyumbani kwao katika mji wa Georgia jana na kukimbizwa hospitali.Inasemekana mtoto huyo amekua akitumia madawa ya kulevya ambayo ndiyo yaliyosababisha kifo cha mama yake
Mume wake Nick Gordon alikutwa akiwa na binti huyo na sasa anahojiwa na polisi kuhusiana na Bobbi Kristina.
Hata hivyo hakukua na maelezo yoyote kutoka kwa daktari baada ya kutokuwepo na msemaji katika hospitali ya North Fulton alikopelekwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:
Post a Comment