Wednesday, February 18, 2015

SERIKALI YA UGANDA YATAKA MABAKI YA IDD AMINI YAREJESHWE NA KUZIKWA UPYA

Story mbili kubwa kutoka Uganda, ipo ya Idi Amin na ishu ya waganga wa kienyeji.

Idi_Amin14Baadhi ya Wabunge Uganda wamepinga kuhusu mpango wa kurudisha mabaki ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Idi Amin Dada kutoka Saudi Arabia na kuletwa nchini humo kwa ajili ya mazishi ya heshima ambapo Wabunge hao wamesema wanaamini Serikali ya Saudi Arabia haiwezi kukubalianana hilo kwa kuwa iko kinyume na dini.
Kulikuwa na taarifa kwamba Serikali ilikuwa katika mchakato wa kuomba mabaki ya mwili wa Idi Amin Dada kufukuliwa na kuletwa nchini humo kwa heshima kama mojawapo ya juhudi za kuleta uwiano, umoja na uridhiano kati ya jamii za Uganda.
Story nyingine kutoka Uganda ni ile inayohusu waganga Kampala kufanya mkutano na kumpitisha Mganga Mkuu Mama Fina ambaye atawaongoza kwa muda wa miaka mitano, huku wakitaka kutambuliwa kwa juhudi zao za kusuluhisha matatizo mbalimbali kwenye jamii.

No comments:

Post a Comment