Kumekuwa
na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na
jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng'oa madarakani rais, Pierre
Nkurunziza.
Rais huyo
ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka katika mkutano wa viongozi wa
kanda,baada ya ndege yake kugeuza kurejea ilikotokea.
Ingawa
askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi
yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya
rais wao,na kwamba udhibiti wa nchi uko mikononi mwao na hasa katika
maeneo muhimu ya mji mkuu wan chi hiyo ,Bujumbura.
Makabiliano
ya risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga .mwandishi wa
BBC aliyeko nchini Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa
limegawanyika pande mbili ,na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa
nchi kwa sasa.
Rais
Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa
uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za
maandamano ambapo watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment