Tuesday, May 5, 2015

CHRIS BROWN AHUSISHWA TENA KATIKA UGOMVI

Chris Brown kahusishwa tena kwenye ugomvi, ishu ilitokea kwenye uwanja wa Basketball !!

chris-brown
Chris Brown staa wa muziki ambae leo ni siku yake kuzaliwa, anatimiza miaka 26.. mara nyingi anatokezea kwenye headlines kubwa, lakini kwenye hizo story zake kubwa nyingi zinahusu ugomvi.
Chris kahusishwa na ugomvi ambao umetokea kwenye uwanja wa Basketball, shuhuda amesema ugomvi wao ulianzia Palms Casino Resort iliyoko Las Vegas na baadae wakaishia kupigana.
Polisi wakasogea eneo lililokua na vurugu hizo na kuchukua maelezo, waliokuwepo wakahojiwa lakini Polisi hawakumkuta Chris !!
Chris kwa sasa yupo Las Vegas.. alialika baadhi ya marafiki zake waje kucheza nae basketball… baadae kuna mtu ambaye hakualikwa lakini aliingia eneo kwenye Uwanja huo wa Basketball. Watu wa Security walikuja kumtoa mtu huyo lakini Chris hakushiriki mabishano wala ugomvi wowote na huyu jamaa.”—alisema Nicole Perna ambae ni msemaji wa Chris Brown.
Mwezi mmoja umepita tangu kesi ya Chris kumpiga Rihanna iishe Mahakamani, kama hii itamkuta kwenye hatia basi muda wowote atarudishwa kwenye headlines zinazohusu kesi.

No comments:

Post a Comment