Wahamiaji wanaosafiri kwenda UlayaVyombo vya habari vya kimataifa vimefahamishwa kuwa wanamgambo wa kundi la Islamic State wanasafirishwa
kwenda barani Ulaya na walanguzi wa binadamu wanaohudumu kwenye bahari
ya Mediterranean.Mshauri wa serikali inanayotambuliwa kimataifa
nchini Libya anasema kuwa walanguzi hao huwaficha wanamgambo ndani ya
mashua zilizojaa wahamiaji.Walanguzi wengine nchini Libya
wanasema kuwa wanamgambo wa Islamic State huwaruhusu kuendelea na
shughuli zao kwa malipo ya asilimia hamsini ya pesa wanazopata.Mashirika
ya mipaka barani ulaya mapema mwaka huu yalionya kuwa wapiganaji wa
kigeni hutumia njia zisizokuwa za kawaida kuingia barani ulaya.
No comments:
Post a Comment