2 wauawa katika shambulizi la bomu Kabul
Watu
wawili wameripotiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mlipuko
kutokea kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege katika mji mkuu wa
Afganistan Kabul.
Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa
kujitolea mhanga alikuwa amelenga wanajeshi wa kimataifa nje ya lango
kuu la uwanja huo wa ndege.
Lango hilo hutumika na maafisa wa kijeshi wa kigeni pekee yao.

Shambulizi hilo linafanyika siku tatu baada ya mwanamgambo mmoja kuwaua watu 14 wakiwemo raia 9 wa kigeni mjini humo.
Hutopitwa na habari inayonifikia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment