Friday, May 15, 2015

HATIMAE MAHAKAMA HISPANIA YAINUSURU LIGI YA HISPANIA

Mahakama kunusuru soka Hispania

Mahakama moja nchini  Hispania imepiga marufuku mgomo uliokuwa unaandaliwa na muungano wa wanamichezo wa  soka nchini humo ambao ulikuwa umepangwa kutekelezwa mwishoni mwa wiki hii.
Mgomo huo ulianza kuhamasishwa wiki iliyopita kufuatia hatua ya serikali ya nchi hiyo kutoa tamko la kurejea upya haki ya urushaji matangazo ya mpira.
Maamuzi ya mahakama hiyo yanatoa nafasi kwa pande zote mbili kuweka taratibu za namna ya kuutatua mzozo huo,ambao unatishia kuuzika mpira nchini humo na hata kuweka shaka ya kutooneshwa kwa mtanange baina ya timu mbili za Atletico Madrid na Barcelona.
Muungano huo wa wachezaji nchini Hispania, umesema kwamba serikali yao imejipanga kuweka mipango ya kisheria juu ya nini cha kufanya na kipi kisifanyike kuhakikisha kila klabu inalipa ushuru kuanzia vilabu vikubwa mpaka vya hadhi ya chini.
Ni halali yako kupata kile kinachonifikia na niko tayari kukutumia kupitia hapa hapa tangakumechablog, usiwe mbani nami

No comments:

Post a Comment