Friday, May 15, 2015

WAHAMIAJI 800 WAOKOLEWA NA WAVUVI WAKATI WAKIZAMA

Wahamiaji 800 waokolewa na wavuvi Indonesia

Zaidi ya wahamiaji mia nane wamewasili katika Mkoa wa Aceh nchini Indonesia baada ya kuokolewa na wavuvi wa mashua yao ilipokuwa ikizama.
Ripoti zasema kuwa mashua nyingine ilirejeshwa Indonesia na jeshi la wanamaji.
Mwandishi wa kituio kimoja nchini Indonesia  amesema kuwa wengi wa watu hao walikuwa wakihitaji matibabu baada ya kukaa baharini karibu miezi mitatu bila maji wala chakula.
Mamlaka za Malaysia imesema kuwa haitaruhusu mashua hiyo kutia nanga katika ardhi yake na kushindwa kutoa sababu huku Umoja wa Matifa unatarajiwa kutoa tamko lake leo hii.
Hutopitwa na habari  yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia kupitia hapa hapa tangakumekuchablog, usiwe mbali nami

No comments:

Post a Comment