Thursday, May 21, 2015

INADAIWA PARACETAMOL IKO NA MADHARA KWA MAMA MJA MZITO

Paracetamol yaathiri uwezo wa kuzalisha:Utafiti

Utafiti umebaini kuwa matumizi ya Paracetamol kwa siku 7 unapunguza uzalishaji wa homoni za kiume na uwezo wa watoto mvulana kuzalisha baadaye
Wanawake wajawazito wanapaswa kuwa na tahadhari zaidi wanapotumia dawa zozote zilizo na chembechembe za Paracetamol.
Utafiti wa Wanasayansi nchini Uingereza umebaini kuwa unywaji wa dawa zenye kiungo cha Paracetamol kwa kipindi cha siku saba unapunguza uwezo wa uzalishaji wa homoni za kiume ''testosterone''.
Homoni hiyo ''testosterone'' ndio inayowezesha kuumbwa kwa sehemu ya uzazi wa kiume .
Sasa madaktari wanashauriwa wasipeane dawa zenye ''Paracetamol'' kwa wanawake waja wazito kiholela.
Na iwapo itawalazimu kupeana dawa hizo basi wanashauriwa kupeana dawa hizo kwa kipindi kifupi ilikupunguza madhara kwa watoto waliotumboni.
Halmashauri inayosimamia matumizi ya madawa nchini Uingereza sasa inasema licha ya kuwa inahujumu kiumbe kilichoko tumboni, Paracetamol ni moja kati ya madawa yenye madhara machache zaidi kwa mama mja mzito na mwanawe.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa onyo kutolewa dhidi ya wanawake wajawazito kupewa dawa zilizo na kiuongo cha Paracetamol.
Awali utafiti wa wanawake waja wazito 2,000, nchini Denmark ulibaini kuwa,wanawake waliomeza dawa za Paracetamol walijifungua watoto waliolemaa katika sehemu ya mfuko wa uzazi- korodani.
Ulemavu huo hatimaye ulijitokeza na kuwa upungufu wa uwezo wao kuzalisha katika maisha yao ya utu uzima.
Paracetamol yaathiri uwezo wa kuzalisha:Utafiti
Aidha inasemekana kuwa wanawake wanaotumia dawa hiyo ya kupunguza maumivu kwa kipindi kirefu wakati wa ujauzito, wanaweza kuathiri mimba zao na hasa kwa watoto mvulana.
Wanasayansi hao wa Chuo kikuu cha Edinburgh, walitumia panya katika utafiti huo.
Shirika linalosimamia maswala ya afya Nchini Uingereza, linasema kuwa wanawake waja wazito wanafaa kumeza tembe hiyo ya paracetamol ikiwa tu wameshauriwa na daktari na pia kwa kipindi kifupi mno.
Dakta Dr Rod Mitchell, aliyeongza utafiti huo anasema kuwa tahadhari kubwa inapaswa kuwekwa inapowadia swala la matumizi ya Paracetamol miongoni mwa wanawake waja wazito.
''utafiti huu unatilia pondo ushauri tuliokuwa nao tayari kuwa chembechembe za dawa hiyo zinaathiri ukuawaji wa sehemu za kiume za watoto wavulana''
Utafiti huo ulifaulu baada ya madaktari kuwapasua panya na kuwapandikiza mimba na kisha wakawapa dawa hiyo kwa siku saba.
Walipoipima iwapo ilikuwa na chembechembe za homoni hiyo ya kiume waligundua kuwa haikuwa nayo.
Hata hivyo walipoipima baada ya siku moja hawakuona tofauti ya viwango ya homoni hiyo muhimu kwa wanaume.
Watafiti hao hata hivyo wanasema ni vigumu kufikia sasa kubaini iwapo athari hiyo ni sawa sawa miongoni mwa wanadamu.
Hilo linatokana na sheria kali zinazozuia utafiti wa aina hiyo.
Licha ya utafiti huu msemaji wa chuo cha afya ya watoto nchini Uingereza Dr Martin Ward-Platt, anaonya kuwa wanadamu hawapaswi kukatazwa kabisa kumeza dawa zilizo na Paracetamol kwa sababu zinasaidia sana kutibu mafua ya mara kwa mara na wakati mwengi kipimo kimoja au viwili vya Paracetamol vinatosha kutibu homa.
Daktari Sadaf Ghaem-Maghami, kwa upande wake ameonya kuwa utafiti huo haupaswi kukubalika pasi na maswali muhimu kuulizwa kuhusu ukweli wake.
''Licha ya kuwa matokeo ya utafiti huu ni mzuri na unavutia ,tunapaswa kufanya utafiti zaidi kwa sababu utafiti huu ulifanyiwa wanyama, Je mwili wa binadamu utaitikia vipimo vya dawa hii kwa njia sawa na hiyo ? alihoji dakta Sadaf.
Utafiti huo umechapishwa katika jarida la kisayansi na utabibu '' Translational Medicine''.
Yote haya yanakuja kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment