Thursday, May 21, 2015

WAGOMBEA URAIS FIFA WAZIDI KUMPA MWANYA BLATTER

FIFA: mgombea mwengine wa urais ajiondoa

Mgombea wa kiti cha Urais wa Fifa Michael van Praag amejiondoa kwenye kinyang'anyiro.
Kujiondoa kwa mwenyekiti huyo wa shirikisho la kandanda la Uholanzi sasa kumewaacha wagombea wawili pekee wanaowania kiti hicho na rais wa FIFA Sepp Blatter.
Van Praag, mwenye umri wa miaka 67, amesema atamuunga mkono Prince Ali Bin Al-Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 29 Mei.
Luis Figo, mwenye umri wa miaka 42,pia anawania kiti hicho
Mchezaji wa zamani wa kiungo kutoka Ureno Luis Figo, mwenye umri wa miaka 42,ni mgombea mwingine katika uchaguzi huo.
Blatter,mwenye umri wa miaka 79, anatarajiwa kushinda muhula wake wa tano akiongoza soka duniani.
FIFA ina wanachama 209 na kila mmoja ana kura moja.
 
Vyama vingi vya soka vilionyesha nia ya kumuunga mkono Prince Ali.
Hata hivyo chama cha soka cha Uskochi awali kilikuwa kimesema kitamuunga mkono Van Praag.
Kujiuzulu kwake kumekuja baada ya mgombea mwingine,katibu mkuu wa zamani wa FIFA, mfaransa Jerome Champagne kujiondoa mwezi Februari.
van Praag anasema kuwa atamuunga mkono Al -Hussein
Uchaguzi huo utafanyika mjini Zurich katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa FIFA.
Mshindi lazima apate theluthi mbili ya kura zote zilizopigwa katika awamu ya kwanza.

No comments:

Post a Comment